Kuna baadhi ya wanawake na wanaume pia hutokewa na tatizo la kupata maumivu kama ya kuhisi kuungua,kuchoma Choma au kuwasha sana baada ya kushiriki tendo la ndoa au wakati wa tendo



Hizi ndio Sababu za Maumivu Yanayotokea wakati wa tendo au Baada ya Tendo la Ndoa

✔️ Kuwa na aleji na Manii, baadhi ya watu wakiguswa na Manii hupata aleji ya haraka mwili unaanza kupambana wenyewe hivyo kumpelekea mtu huyu kuanza kuhisi kuwashwa au hali ya moto moto sehemu zake za siri. 

✔️ Kuwa na Ugonjwa wa UTI, fangasi na P.I.D huathiri mfumo wa mkojo na kufanya maumivu makali wakati wa tendo au wakati wa kukojoa. 

✔️Mwanamke  Kutokuwa na vilainishi ( Ute Ute), Kwa kawaida uke unatengeneza maji maji ambayo huwa ni kilainishi wakati wa tendo, hivyo baada ya kuandaliwa na kupata hisia hutoa maji ikiwa mwanamke hutaandaliwa vizuri akishiriki tendo anapata maumivu pengina na michubuko.

✔️ Mwanaume kuwa na maumbile makubwa, maumbile makubwa zaidi yanaweza kumuumiza mwanamke wakati wa tendo.Hii piia inaweza kutokea endapo mwanamke ana kuta za uke zilizobana sana.

✔️ Tendo kufanyika kwa muda mrefu, zaidi ya nusu saa au bao nyingi zaidi, pia hii inaweza kuleta hali ya Maumivu Kwa wote wawili. Hali hii inapelekea kukauka kwa kilainishi (Ute Ute), hivyo ule msuguano hufanyika kati ya nyama za uke na uume.

✔️ Namna tendo limefanyika, mfano kubadilisha badilisha mikao, vurugu au kutumia nguvu nyingi sana wakati wa tendo hupelekea kuleta maumivu badala ya kufurahia tendo.

✔️ Kuwa na Magonjwa ya zinaa,  kwani huathiri mirija ya uzazi na kupelekea kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

✔️ Fangasi, huathiri sana sehemu za Siri na kusabababisha miwasho  inapelekea Kuta za uke kuvimba na kuota vipele ambavyo huweza kupasuka wakati wa tendo la ndoa na kukufanya upate maumivu makali.

✔️ Kuwa na majeraha katika viungo vya Uzazi.

✔️ Mwanaume kutotahiriwa na mwanamke kukeketwa.

✔️ Kuwa na Uvimbe katika viungo vya Uzazi pia inaweza kuwa kati ya sababu zinazopelekea maumivu wakati wa tendo la ndoa hasa Kwa Wanawake.

Ikiwa una tatizo katika uzazi na unahitaji msaada kutoka kwetu basi wasiliana nasi sasa.

Tunapatikana Mbeya, Mbalizi stendi ya tunduma ya zamani barabara ya kuelekea kanisa la LAST CHURCH


BOFYA HAPA KUWASILIANA NASI