H.PYLORI



Yawezekana umewahi kwenda hospitali ukisumbuliwa na dalili za vidonda vya tumbo na kufanyiwa vipimo kisha daktari anakwambia una bacteria wanaoitwa h.pylori. Kama bado basi usichukulie rahisi maana athari yake ni kubwa sana.

Baadhi ya athari zinazitokana na bacteria hawa huweza kusababisha saratani ya tumbo kama tatizo halitatibiwa vizuri na Kwa haraka.

Maelezo yafuatayo tumeongelea nini hasa maana ya h.pylori, jinsi wanavyo sababisha vidonda vya tumbo na saratani ya tumbo, pamoja na tiba za asili za kuua bacteria hawa.


H.pylori nini hasa?




H. pylori ni kifupi na helicobacter pylori. Ni aina ya bakteria ambayo huingia kwenye mwili na kujificha ndani ya mfumo wa chakula. Nikisema mfumo wa chakula hapa ieleweke kwamba ni kuanzia mdomoni unapobugia chakula chako mpaka kwenye tundu la haja kubwa ambapo unatoa kinyesi.

Hivyo kumbe bakteria hawa wanapatikana hata mdomoni na wanaweza kuambukizwa kwa mdomo pia. Sasa kutokana na bacteria hawa kuwa na uwezo wa kujishikiza kwenye kuta za tumbo bila kuathiriwa na tindikali inayomwagwa tumboni, huweza kusababisha vidonda vya tumbo na saratani pia.

Nafahamu kuwa uliwahi kuambiwa kwamba vidonda vya tumbo husababishwa na tabia ya kutokula kwa wakati au kukaa na njaa kwa muda mrefu au kuwa na msongo wa mawazo kupitiliza.


Nini husababisha H.Pylori kuingia kwenye mfumo wa chakula?



Ukirudi mwanzo nimesema bakteria hawa hupatikana kwenye mfumo wa chakula, kuanzia mdomoni hadi kwenye tundu la haja kubwa. Sasa nini kinapelekea mpaka hawa bacteria kumuingia mtu.

Chanzo cha kupata bacteria huwa ni kupitia mdomo. Bacteria hawa hupatikana kwa kiasi kikubwa kwenye maji, hivyo kama maji unayokunywa hayajatibiwa au kuchemshwa basi hatari ya kupata bacteria hawa ni kubwa zaidi.

Chakula pia unachokula kama kimepata maambukizi ya hawa bacteria basi ukila unameza na hawa bacteria. Chanzo kingine ni kupitia ngono. Najua kuna kundi kubwa la watu wanaopata maambukizi ya bacteria kupitia kufanya mapenzi kunakohusisha midomo ikiwemo kunyonyana ndimi au denda.

Hivyo hakikisha mpenzi wako yuko salama kabla hujamuamini manake utajiepusha si tu na h.pylori bali pia na ugonjwa wa homa ya ini yaani Hepatatis B.

Vipimo vya kugundua H.Pylori

Kwa bahati nzuri hospitali zetu nyingi zinatoa huduma ya vipimo kwa gharama nafuu sana. Hivyo kama unapata dalili ambazo nitazielezea hapo chini hakikisha unaenda hospitali kupata vipimo ili uwahi tiba mapema.


Dalili hizi kuwa na H.pylori/ Vidonda vya tumbo 

👉kujiskia tumbo limejaa muda wote hata kama umekula kidogo tu,

 đꑉkutapika na kupata kichefuchefu mara kwa mara unapokula au hata muda ambao hujala chakula.

👉kushuka kwa uzito kwa kasi bila sababu ya msingi,

👉mwili kuwa mzembe na kuchoka choka sana mara Kwa mara

👉Maumivu makali ya tumbo, kiungulia, na

kupoteza hamu ya chakula.

👉Miguu kufaa ganzi na kuhisi Kama inachoma choma na kuwaka moto

Kama tayari uliwahi kuugua vidonda vya tumbo hapo nyuma basi daktari ataangalia rekodi yako ya nyuma na kupendekeza aina ya matibabu yanayokufaa.


Ni madhara gani utapata endapo hutatibiwa vizuri?

Kama utaugua H.pylori kwa muda mrefu pasipo kupona vya kutosha, kuna hatari ya kuta za kwenye utumbo kutoboka na hivyo kuruhusu sumu kuingia kwenye damu. ikitokea hali hii kila chakula utakachokula waweza kutapika na kuharisha, mwili utadhoofu sana na kilo kupungua kwa kiasi kikubwa.

Pia kuna hatari ya kupoteza maisha, kupata saratani/kansa ya tumbo na utumbo, endapo tatizo litakusumbua kwa muda mrefu sana.


Tiba kwa H.Pylori

Kwenye tiba ya kisasa (conventional medicine)

Hatua ya kwanza daktari wako atakupatia dawa ya kwanza ni kwa ajili ya kuua hawa bacteria wa h.pylori. Hatua ya pili ni kutumia dawa kwa ajili ya kupunguza tindikali inayomwagwa kwenye kuta za tumbo.

Baada ya hapo itahitajika kufanya ufatiliaji juu ya mwenendo wa tatizo lako ili kuhakikisha kuwa linaisha kabisa. Japo kwa wagonjwa niliowahudumia ni wale waliotumia tiba ya hospitali bila mafanikio. Tiba ya hospitali inaonekana kuwa na ufanisi mdogo kwa wagonjwa wengi


Tiba asili ya h.pylori (functional medicine)

Bacteria hawa wanapotibiwa mara kwa mara kupitia tiba za kisasa zinazotolewa hospitali hufikia kipindi wanakuwa sugu yaani hawasikii dawa. Nimekuwa nikipata kesi kama hizi wagonjwa wengi wanasumbuliwa na vidonda vya tumbo sugu ambavyo haviponi, vimechukua miaka mpaka mitano, mpaka wengine hupoteza tumaini.

Basi unaweza kutumia tiba zetu za asili ambazo ziliweza kuua bacteria hawa kwa wagonjwa wote tuliowahi kuwahudumia. Njia za asili hulenga katika kuua bacteria wabaya tu na kaacha bacteria wazuri. Kumbuka miili yetu imeumbwa na bacteria wazuri na wanahitajika ili kuweka msawazo.


Muhimu upimwe kwanza

Ni muhimu kufika hospitali kupata vipimo na ufatiliaji wa daktari juu ya tatizo lako. Tumia tiba asili kwa uangalifu na kwa kufata ushauri wa mtaalamu wa tiba asili. Usinunue kila dawa mtaani zinaweza kuongeza tatizo badala ya kutibu.

Lakini pia unaweza kuwasiliana nasi MAYILA HERBAL CLINIC kwa ushauri wa kiafya, huduma ya tiba na elimu ya mpangilio wa lishe ili kutibu matatizo mbalimbali ya kiafya. 


Pia Unaweza kutumia dawa yetu inayoitwa TUMBO MUJAARAB ni dawa ya siku 7 ambayo itakusaidia kusafisha mfumo wa chakula, na kuua bacteria wabaya. Ni dawa ya asili yenye mchanganyiko wa zaidi ya aina 16 za mitishamba zenye uwezo mkubwa wa kutibu vidonda vya tumbo na matatizo ya tumbo Kwa ujumla. Utazitumia dawa zetu kwa muda wa wiki moja na kupona ugonjwa wako.


 BONYEZA HAPA KUWASILIANA 

NA DR. MAYILA KWA MSAADA ZAIDI